You are currently viewing Balozi Karume: Viwanja vya Ndege Zanzibar sasa mali ya Dubai

Balozi Karume: Viwanja vya Ndege Zanzibar sasa mali ya Dubai

Kauli ya Balozi Ali Karume kuhusu ufisadi unaoendelea kuitikisa Zanzibar. Safari hii kagusia viwanja vya ndege. Balozi Karume anasema kitendo cha viwanja vya ndege kupewa mwekezaji DNATA na Rais Mwinyi kupewa ubia katika kampuni hiyo ni sawa na usaliti na uuzaji wa nchi kupitia Ikulu.

Balozi Karume ametoa pia maoni yake kuhusu ubinafishwaji wa bandari na kupewa Wafaransa. Nyaraka za siri zinaonesha Wafaransa wameshikiana na Rais Mwinyi na Mbunge Tourky kugawana bandari licha ya uwekezaji wa mabilioni ya walipakodi wa Zanzibar. Soma zaidi www.aglzanzibar.com! Mfaransa mbaguzi anayepingwa kila kona ya Afrika leo kapewa mjeledi kutimua wafanyakazi bandari ya Zanzibar kisa bwana mkubwa karambishwa asali ya asilimia thalathini za kampuni. CCM mnasubiri 2025 kumuondoa huyu bwana lakini mnaweza kukuta hali isiyotamanika.

Shirikisha