You are currently viewing Nyaraka: Familia ya Mwinyi yajitwalia eneo la umma kujenga mall Zanzibar

Nyaraka: Familia ya Mwinyi yajitwalia eneo la umma kujenga mall Zanzibar

Mchoro unaonesha mall mpya inayokwenda kujengwa hapa Zanzibar yenye jina Mwinyi Mall. Msimamizi wa mradi ni ndugu yake Rais Hussein Mwinyi kwa niaba ya familia nzima ya Mwinyi. Rais ametumia madaraka yake isivyo maadili kujipa ardhi ya mradi. Eneo la mradi la magereza (Kiinua Mguu Kilimani) Unguja. Katika sinema alizocheza Rais Mwinyi kupata eneo hilo alipokua anataka kuuza nyumba za Kilimani kumbe tayari kishapanga kujimegea na eneo la magereza ambalo lipo upande wa pili wa barabara. Hapo ndipo anataka kujenga Mwinyi Mall.

Baada ya gereza iko baa maarufu Kwa Raju ambayo kwa ukwasi alonao Hussein Mwinyi pia kainunua. Baada ya Bar ya Raju lipo eneo la faya ambalo nalo kishalichukua. Baada ya eneo la faya iko nyumba ya baba yake Rais Mwinyi, Mzee Mwinyi. Anataka kuunganisha na eneo la faya na Bar ya Raju kujenga nyumba za biashara kwa pesa za wizi za alofanya na anaoendelea kufanya dhidi ya Wazanzibari.

Kwa ufupi anajijengea kijiji kifisadi hapa Zanzibar. Kama mnakumbuka Mzee Baraka Shamte alisema pia kwa nyuma ya nyumba ya Mzee Mwinyi iko nyumba ya Maparisi ambayo pia bwana mdogo kishachukua kwa kubadilishana na bwana Muzammil na kumpa nyumba mbili za serekali za Mji Mkongwe.

Pakua nyaraka za mchoro wa mall hiyo HAPA. Tembelea tovuti ya mall mpya kwa kubofya www.mwinyimall.com

CCM mnasubiri hadi 2025?

 

Shirikisha