You are currently viewing Mabadiliko TISS ni ishara ya makubwa yajayo Zanzibar

Mabadiliko TISS ni ishara ya makubwa yajayo Zanzibar

Majuzi Rais Samia kafanya mabadiliko makubwa na ya kihistoria TISS kwa kumuondoa DGIS Massoro na kumuweka Balozi Ali Siwa. Baadhi ya wachambuzi wanasema mabadiliko hayo yanagusa siasa za bara na Uchaguzi 2025. Wapo wanaosema yanagusa marekebisho yanayoendelea ili kuimarisha idara hiyo nyeti nchini ilai wapo wabobezi wanaosema ni ishara ya mabadiliko makubwa yanayokwenda kutokea Zanzibar. Balozi Ali Siwa ni mbobezi wa intelijensia kwenye kipindi cha mpito. Faili lake linasema alijiunga na TISS mwaka 1977 na kituo chake cha mwanzo kilikuwa Zanzibar. Hiyo ilikuwa ni miaka mitano tu baada ya kifo cha Karume ikiwa na maana kwamba huyu bwana ni mjuvi wa nini cha kufanya Rais wa nchi anapofia madarakani, hasa kwa Zanzibar ama nchi inaongozwaje ukiwa na Rais wa mpito wa kipindi kimoja. Miaka hiyo akiwa Zanzibar ni moja ya makachero ambao taarifa zao zilisaidia sana kuunganisha ASP na TANU mwaka 1977 na baadaye mwaka 1984 kumuondoa Aboud Jumbe madarakani alipotikisa nyavu kutaka Zanzibar ijitenge. Siwa amekuwepo kwenye operesheni za mabadiliko yote makubwa Zanzibar kuanzia kumuondoa Jumbe mwaka 1984, Maalim Seif kufungwa gerezani kwa uhaini,kuporwa kwa uchaguzi mkuu zanzibar 1995 hadi mauaji ya 2011.

Majasusi wote wakubwa waliowahi kuongoza TISS wanapimwa kwa uwezo wao wa kuituliza Zanzibar. Sasa hivi Zanzibar tuna Rais bilionea, aliyechuma mabilioni ya dola kwa rushwa na ufisadi ndani ya muda mfupi, anamiliki mahoteli, mifumo ya kukusanya mapato, hisa za bandari na kadhalika. Bahati nzuri hana hiba wala historia ya mzee Karume, hana ushawishi alokuwa nao mzee Jumbe na wala damu ya kimapinduzi. Tuna Rais mradi (project), anayejua aliwekwa Zanzibar kwa mpito mpaka pale Wazanzibari wenyewe hasa ndani ya CCM watakapowekana sawa na kuamua nani awe Rais wao. Uteuzi wa Balozi Siwa ni ishara kubwa kuwa siku za bwana mdogo visiwani Zanzibar zinahesabika.

Shirikisha