You are currently viewing INAHUZUNISHA:HUSSEIN MWINYI NA TOUFIQ TURKY WALIVYOSHIRIKIANA NA WAFARANSA KUJIMILIKISHA BANDARI YA MALINDI ZANZIBAR!

INAHUZUNISHA:HUSSEIN MWINYI NA TOUFIQ TURKY WALIVYOSHIRIKIANA NA WAFARANSA KUJIMILIKISHA BANDARI YA MALINDI ZANZIBAR!

Wakati nchi nyingine zinahangaika kuboresha bandari zao,hapa Zanzibar Rais Mwinyi na rafikiye Mbunge wa Mpenda bwana Toufiq Turky wamejimilikisha bandari ya Malindi na sasa kila pasenti ya senti inayokusanywa pale inakwenda kwao. Kwa ufupi kila unacholipa kwa matumizi ya bandari asilimia thelathini inakwenda kwa Mwinyi na Toufiq Turky.

Ngoja nikufahamishe vizuri ….
Utawala wa Dokta Shein na watangulizi wake waliwekeza mamilioni ya dola kuboresha bandari ya Malindi. Kaja Hussein kaona watangulizi wake wote walikuwa hawana akili, akajizawadia bandari!. Wakasuka dili yeye na Toufiq wakaiuza bandari nzima nzima kwa kampuni ya Bolore na fedha uwekezaji wote wa SMZ ambayo ni jasho la wazanzibari ikawa ndio mchango wa hisa za Hussein na Toufiq.Kodi yetu Wazanzibari mamilioni ya dola iliyotumika kununua mitambo mipya kuendeshea bandari imegeuzwa kuwa pesa ya manunuzi ya hisa kwa Hussein na Toufiq.Mgao wao wawili ni asilimia thelathini na mwekezaji asilimia sabini.Wasojua vizuri Bolore pia ni Wafaransa, wanaotafuna Afrika Magharibi,wale waliofurushwa na kiongozi kijana Ibrahim Traore kule Burkina Faso majuzi!. Sisi Rais wetu kapewa chake kawaingiza ukumbuni!

CCM huyu bwana mlimleta Zanzibar kuifanya kichaka cha wizi na ufisadi ama kuongoza?Zanzibar ni ya Wazanzibar na kama ilivyo historia ya Zanzibar laana hii ya kufukarisha Wazanzibari haitapita bila madhila kwa wahusika!!

Shirikisha