You are currently viewing Jionee ufisadi wa Rais Mwinyi unavyozidi kuifukarisha Zanzibar

Jionee ufisadi wa Rais Mwinyi unavyozidi kuifukarisha Zanzibar

Awali ya yote nianze kwa kumshukuru Allah (Subhaanahu wa Taala) na kumtakia rehema bwana Mtume Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Hii ni habari fupi lakini yenye kusitikitisha sana kwa mustakabali wa Zanzibar yetu. Unaposoma habari hii nakusihi washirikishe ndugu zetu Wazanzibari popote walipo wapate kufahamu madhila ambayo nchi yao inapitia chini ya uongozi wa Rais Mwinyi. Hii ni habari moja tu kati ya mamia ya habari za aina hii ambazo mtandao huu utaendelea kuziweka bayana kwa umma wa Wazanzibari.

Benki ya Dunia ina mahakama yake ya kusuluhisha mashauri ya mikataba ya kimataifa kati ya nchi na nchi ama nchi na makampuni ya kimataifa. Hapa Zanzibar Mwenyezi Mungu alitujalia kupata kampuni ya Pennyroyal iliyokuja na kununua ardhi Zanzibar ikitaka kujenga mji mkubwa wa utalii Matemwe, hekta 411. Ilikuwa fursa ya ajira zenye kubadili maisha kwa maelfu ya Wazanzibari. Alipoingia Rais Mwinyi akaona Wazanzibari hawastahili ajira hizo wala maisha bora kutokana na mradi ule. Akataka amegewe yeye ardhi ile na genge lake, apewe bure bure hekta 80 ili aweze kuruhusu mradi kuendelea.

Sasa dhulma wamezoea kutufanyia sisi wanyonge ila kwa wawekezaji hawa wakamgomea wakafungua kesi hapa Zanzibar na kwenye hiyo mahakama ya benki ya Dunia. Kesi inaelekea sasa wanakwenda kushinda na wanadai shilingi trilioni 2 unusu kama fidia ya Mwinyi kuvuruga mradi ule wa neema kwa maelfu ya masikini wa Zanzibar. Trilioni mbili unusu wanayodai fidia ni sawa na pesa ya bajeti nzima ya Zanzibar kwa mwaka. Nani analipa fedha hizi? Ni sisi Wazanzibari. Tunakwenda kutumia bajeti ya mwaka mzima kulipa fidia kwa tamaa za Rais Mwinyi na kikundi chake kidogo kama kile cha futungo Angola kilichofisadi nchi nzima chini ya Rais Dos Santos. Kama tulivyosema mwanzo hili ni moja kati ya madudu mamia yanayoendelea kufanywa na mtu huyu na kundi lake dhidi ya Zanzibar? Nchi inafisadiwa utadhani Rais kaja talii achukue chake arudi atokako.!

Shirikisha